Mkali wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim ‘Wizkid’, amedai anatarajia kufanya makubwa 2017 na hana mpango wa kuangalia aliyoyafanya 2016 .

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26, alifanya makubwa mwaka 2016 kwa kufanya kazi na wasanii wakubwa wa muziki duniani akiwemo, Drake na  Chriss Brown.

”Mwaka jana nilifanya makubwa pamoja na kununua nyumba nchini Marekani, lakini mafanikio hayo si kitu chochote kwangu, natarajia kufanya makubwa zaidi kwa mwaka huu.

”Kwa sasa nipo katika mapumziko hadi Februari mwaka huu, sina mpango wa kuangalia nilipotoka, nataka niwe kama nimezaliwa upya huku nikiwa na kiu ya mafanikio,” aliandika Wizkid.

Ferooz awaomba wasanii kutojihusisha na madawa ya kulevya
Ally Star: Taarabu itakufa tusipoisaidia