Staa wa muziki kutoka Nchini nigeria Ayodeji Ibrahim maarufu kama Wizkid aneyetamba na wimbo wa Joro amethibitisha kuwepo kwenye grand final ya wasafi festival katika viwanja vya posta kijitonyama usiku wa leo Jijini Dar es Salaam.

Staa huyo amethibitisha kupitia insta srory ya ukurasa wake wa instagram kwa kuandika ”Tanzania see you”

Kwake ni mara ya pili kuja kutumbiza Tanzania ambapo kwa  mara ya kwanza alitumbuiza katika tamasha la Fiesta mwaka 2016 na mwaka 2019 anatumbuiza katika tamasha la wasafi Festival.

Staa huyo atakamilisha orodha ya mastaa wawili kutoka nchini Nigeria ambapo tayari Tiwa savage ameshawasiri nchini jana usiku kwaajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

Aidha msanii kutoka nchini Congo Innos B anayetamba na wimbo wa Yope aliomshirikisha Diamond Platnumz anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo huku akiungana na wasanii wengine wa bongo fleva.

 

 

Jafo asema uchaguzi upo palepale
CHAUMA waunga tela kususia uchaguzi

Comments

comments