Muigizaji wa Filamu za bongo ambaye kwa sasa amejikita katika sanaa ya mitindo, Jackline Wolper maarufu kama Wolperstylish, amewaomba watanzania kushirikiana kumrudisha kwenye mstari msanii Kabula ambaye kwa sasa hali yake si shwari kiafya.

Wolper kupitia mtandao wake wa instagram amewaomba watanzania pamoja na wasanii wa Bongo Movie kushikamana na kumuokoa msani mwenzao jini Kabula ambaye inasemakana anaugua ugonjwa wa akili.

Jini Kabula ni msanii wa Filamu za kibongo ambaye alipata umaarufu wake kupitia tamthilia ya jumba la dhahabu ambapo msanii huyu alivaa uhusika wa jini, na ndipo jina lake na umaarufu wake ulipoanza kukua, filamu hiyo ilikuwa ikioneshwa katika kituo cha chaneli ta taifa cha TBC.

”kabula wangu natamani niongee mambo mengi juu  yako lakini natamani hata kukusaidia urudishe akili yako swali ni kwamba nimechelewa, nakama nimewahi je nitafanikiwa kweli, ameuliza Wolper.

Wolper amesema kuwa kama ni kweli Kabula anauugua ugonjwa wa akili hawana budi kumsaidia kwani wataalamu wapo wengi wakulimaliza tatizo lake na akawa sawa.

Hivyo amewaomba watanzania kutoa mchango wa maoni na ushauri kupitia namba 0765776776 ili kumsaidia Kabula kurudi katika hali yake ya kawaida.

Aidha Wolper amesema kuwa sasa yupo safarini ila matumaini yake akirudi safarini ataelekea nyumbani kwa Kabula kumjulia hali na kuzungumza nae machache.

Amemaliza kwa kusema ” Bongo movie tumfwate alipo jamani tujue tunamsaidiaje”.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 3, 2017
Video: Wabunge waliotimuliwa CUF watinga mahakamani