Muigizaji mahiri kutoka kwenye tasnia ya filamu Tanzania Bongo, Jaqueline Wolper na mchumba wake Rich Mitindo wameutangazia ulimwengu kuwa wanatarajia mtoto wa pili katika familia yao.

Mitindo ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake maalum wa mtandao wa Instagram, akitangaza rasmi kwa mashabki wa familia yao kuwa mkewe ni mjamzito na kwamba wanasubiri kumkaribisha mtu mpya katika familia yake.

“Asante Mungu kwa hii zawadi nyingine, Wakati tulipofikiri kwamba tumebarikiwa mtoto wa kwanza ajabu Mungu Kaonyesha miujiza yake nakutupa furaha nyingine.

Nasubiri kwa hamu ujio wako, karibu sana mwanangu, Mama yako anakupenda sana, Pia mimi na Kaka yako maombi yetu yapo juu yako,”. aliandika Rich.

Taarifa iliyoambatana na pongezi kutoka kwa watu mbali mbali mashuhuri wenye kuwatakia heri, Ikiumbukwe Wolper na Mitindo walimkaribisha mtoto wao wa kwanza mapema mwaka 2021.

Maaskofu wasusa ibada kupinga mwaliko Viongozi mashoga
Bien wa Sauti Sol aonyesha jeuri ya pesa