Muigizaji wa filamu, Jacqueline Wolper ambaye kwa sasa ameamua kugeuzia kisogo sanaa hiyo na kugeukia katika sanaa ya mitindo na kuwa mmiliki wa duka kubwa la nguo Wolperstylish, penzi lake jipya limeingia dosari baada ya aliyekuwa mpenzi wa mpenzi wake wa sasa kujitokeza na kumtupia kashfa za kumuibia bwana huyo.

Kabla ya kuwa na mpenzi huyo maarufu kama Brown,  mwanadada Wolper alizama kwenye dimbwi la mapenzi na mmoja ya wasanii chini ya Lebo ya Wasafi, Harmonize, lakini baada ya penzi hilo kusambaratika Harmonize akaopoa mtoto wa kizungu na kumjaza kibendi.

Wakereketwa hawakutaka kulaza damu, wamemtafuta Wolper juu ya tuhuma hizo za kuiba mume wa mtu na Wolper alionesha kushitushwa na taarifa hizo kwani anachojua yeye mchumba wake huyo mpya hana mpenzi mwingine zaidi yake na waliopo ni wale ambao amekwisha achana nae.

“Kinachonishangaza ni kitendo cha mimi kuwa naye tu ndiyo watu wanaanza kuibuka na kusema eti ana mke, duh!” amehoji Wolper.

Katika kutengeneza usawa wa habari, media zilimsaka kijana mpya wa Wolper maarufu kama Brown na kumuhoji juu ya tetesi hizo, Brown alisikitishwa na madai hayo na kudai kuwa hana msichana mwingine yeyote zaidi ya Wolper na wengine ambao ni ma ex wake.

“Sina mwanamke mwingine niliyenaye kwenye uhusiano zaidi ya huyo unayemjua, ninachojua ni kwamba mwanamke aliyeibuka na kudai mimi ni mumewe huyo ni ex wangu ambaye tuliachana kitambo sana hata wakati sijawa na uhusiano na mwanamke niliyenaye sasa”. amesema Brown.

Hivyo aliwaomba wanawake kutulia kwani yeye sasa hana mtu mwingine yeyote zaidi ya Wolper.

Afande Sele: Ofisi ya chama cha soka Tanzania aibu yetu
Mbowe: Upinzani ni wito