Baadhi ya mashabiki wa wapenzi hao wawili Wolper na Harmonize waliandika maoni hayo baada ya kile kilichotokea katika mitandao ya kijamii ambapo Wolper alipost picha ya Harmonize na kuambatanisha ujumbe mzito ulioleta tafrani kwa baadhi ya mashabiki wanaokubali na wale ambao hawakubali mapenzi yao.

Ambapo kutokana na maneno aliyotuma Wolper kwenye mtandao wake wa kijamii inasemekana dhahiri wapenzi hawa wawili, penzi lao limefika tamati, baada ya Wolper kuamua kuweka wazi kuwa uhusiano wao umefika mwisho na kuandika ujumbe kwa kumwambia laazizi wake Harmonize kuwa yeye si mtoto mdogo na anaakili timamu.

Hakuishia hapo Wolper alisisitiza kwenye mtandao wake kuwa ”endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @Harmonize_tz i hate you”.

Kutokana na post hiyo baadhi ya mashabiki walitoa maoni tofauti tofauti wengine walidai wanatafuta kiki wakati wengine walidai huenda wakawa wanatengeneza video, na wale ambao walikuwa hawapendi mahusiano yao walimuunga mkono Wolper na kuandika Harmonize sio type yake.

picha ya Harmonize iliyoambatanishwa na maneno hayo mazito haikuchukua muda kukaa kwenye akaunti ya Wolper ikafutwa japokuwa wapo walioweza kuinasa na kuisambaza.

 

Samia suluhu atoa agizo kwa majaji nchini
Belle 9: Diamond ni mdogo wangu siwezi kumuiga kwa chochote