Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Arsenal, Ian Wright amemshangaa kocha wa Klabu hiyo Arsenal Wenger  huku akimtaka aondoke Klabuni hapo kwa sababu amekosa mbinu za kuisaidia timu hiyo.

Wright amesema kuwa haiwezekani kwa kocha mwenye malengo mazuri na klabu yake kuendelea kuwaruhusu wachezaji kuondoka kwani kufanya hivyo ni kuzidi kuididimiza klabu hiyo na kurudisha nyuma maendeleo ya klabu.

Ian Wright ambaye alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha Wenger walioshinda kombe la FA mara mbili mwaka 1997-98 amesema kuwa matatizo hayo yote yanasababishwa na kocha huyo.

”Ni kwa manufaa na heshima yake mwenyewe ni ndoto kubwa sana kwa sasa kuweza kufikia malengo ya kuweza kutoa ushindani wa kuchukua kombe la ligi kuu ya Uingereza, mimi ningependelea tu aondoke,” amesema Wright.

Hata hivyo, Wright ameshangazwa na ripoti kwamba Arsenal imekubali ombi la Chelsea kumsajili Alex Oxlaide-Chamberlain huku akisema kuwa Alexis Sanchez naye anatarajia kuuzwa kabla ya dirisha la uhamisho kumalizika siku ya Alhamis.

Rais Magufuli alivyotembelea makao makuu ya Kakukuru
Video: Kuna watu wanataka kuniua - Maalim Seif, Mgomo wa Mawakili pasua kichwa