Mabingwa wa soka nchini Misri Al Ahly, huenda wakafuzu kucheza hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, endapo wataifunga Wydad Casablanca katika mchezo wa jumatano ambao utapigwa nchini Morocco.

Kama waarabu hao wa Misri watafanikisha mpango wa kutinga kwenye hatua ya mtoano, itakua ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo, tangu walipofanikiwa kutwaa ubingwa wa nane wa Afrika 2013 kwa kuifunga Orlando Pirates ya Afrika kusini.

Al Ahly walishindwa kuingia nusu fainali miaka miwili iliyofuata, na msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya tatu hatua ya makundi kabla ya kucheza nusu fainali.

Kocha wa Al Ahly Hossam El Badry ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa klabu huyo ya jijini Cairo, amewataka mashabiki wao kuandamana na kikosi bila kuhofia lolote, zaidi ya kuamini wanakwenda ugenini kufanya vyema siku ya jumatano.

Amesema anawaamini sana mashabiki wa Al Ahly juu ya mapenzi waliyonayo, na katika mchezo ujao dhidi ya Wydad Casablanca watakua na kikosi chao bila kuchoka.

El Badry ameongeza kuwa, lengo lao katika mchezo huo wa jumatano ni kuhakikisha wanashinda kwa namna yoyote, na uwezo huo anaamini upo miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi chake.

Michezo mingine ambayo itachezwa juma hili ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Group A. 

Jumanne: Al Merrikh v Ferroviario Beira

Jumatano: Al Hilal v Etoile du Sahel

Group B:

Jumatano: Al Ahly Tripoli v CAPS Utd (utacheza nchini Tunisia kwa sababu za kiusalama).

Jumatano: USM Alger v Zamalek

Group C: 

Jumanne: AS Vita Club v Saint George

Jumatano: Wydad Casablanca v Al Ahly

Group D

Jumanne: Coton Sport v Zanaco

Jumatano: Esperance v Mamelodi Sundowns

Video: Rin Marii amshauri Diamond kuhusu Tiffah na Muziki, afunguka kuhusu mikakati yake
Video: Waziri Mkuu azindua Kamusi Kuu ya Kiswahili