Mkali wa ‘Achia Body’, Ommy Dimpoz anajiandaa kuwashika tena mashabiki wake waliompokea kwa kishindo miaka kadhaa iliyopita alipotambulisha ngoma yake ya ‘Nainai’ akiwa na Ali Kiba.

Ikiwa ni miaka mitano imepita, Ommy Dimpoz amempa shavu tena Ali Kiba kwenye wimbo wake mpya utakaotoka hivi karibuni ambao yeye amedai ni ‘hatari nyingine’.

Akifunguka hivi karibuni katika mahojiano na kituo cha runinga cha The Citizen nchini Kenya, Ommy Dimpoz aliwataka mashabiki wake kusubiri kishindo cha ujio wa ngoma hiyo na kwamba atafanya tour maalum kuutambulisha nchini Kenya akiwa na ‘King Kiba’.

“Hii ninawapa kama siri, hata Tanzania hawajui… wimbo niliofanya na Ali Kiba ni mkali na tayari tumeshakamilisha kushuti video ambayo pia ni nzuri sana. Tutakuja kuitambulisha pia hapa Kenya,” alisema Ommy Dimpoz.

Aliwataka mashabiki wake kujiandaa kusikiliza wimbo mkubwa kwakuwa Ali Kiba na yeye wanapokutana inakuwa hatari nyingine.

ommy-dimpoz-na-kiba

Mwanzoni mwa wiki hii, Msanii huyo alipost baadhi ya picha zinazoonesha utayarishaji wa video ya wimbo huo ulivyokuwa.

Madereva wa Malori wa Tanzania, Kenya waliotekwa Kongo waokolewa
Hans van Der Pluijm: Tutachukua Chetu Mapema