Uongozi wa Azam FC umekanusha taarifa za Beki wao kutoka nchini Ghana Yakub Mohamed kuwa mbioni kutua Young Africans.

Azam FC wamekanusha uvumi huo, baada ya kuona unaendelea kusambaa kwa kasi kubwa katika mitandao ya kijamii.

Taarifa kutoka Azam Complex Chamazi zimesema kuwa, mpaka sasa hawajapokea ofa yoyote kutoka Young Africans inayomuhusu Yakubu.

Hata hivyo tetesi zinaeleza kuwa mkataba wa Azam FC na Yakubu unaisha Novemba 2021, hivyo Young Africans huenda wakatumia nafasi hiyo kuanza chochoko za kumsajili.

Kanuni za usajili zinatoa nafasi kwa klabu yoyote duniani kufanya mazungumzo na mchezaji aliesaliwa na mkataba wa miezi sita.

Tetesi za mchezaji huyo kutua Jangwani zinasema kuwa Young Africans imejipanga kumsajjli kwa mkataba wa miaka miwili.

RC Makala aruhusu biashara soko dogo la Kariakoo
Rais Samia azungumza na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya