Jose Mourinho hataki Ryan Giggs abaki Manchester United kama msaidizi wake kwa sababu ana wasiwasi kuwa huenda akawa hasimu wake baadaye (Times)

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, 27, anazidi kukosa utulivu Ujerumani na huenda akafikiria kuhamia EPL (Mail)

West Ham wanajiandaa kupanda dau la pili la pauni milioni 8 kumsajili winga wa Bournemouth Matt Ritchie, 26 (Telegraph)

Meneja wa Bournemouth Eddie Howe hafuatiliwi tena na Southampton, lakini huenda kocha wa zamani wa Roma Rudi Garcia akapewa kazi hiyo (Telegraph)

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Ham Dimitri Payet, huku wapiga nyundo wakizidi kuona itakuwa vigumu kumzuia kuondoka (Mirror).

Licha ya habari kuzagaa wamiliki wa Liverpool wamesema hawana mpango wa kuuza timu hiyo kwa wawekezaji kutoka China, na kusema bei ya pauni milioni 700 ni ya „chini kidogo”.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kumpa nafasi zaidi Juan Cuadrado, 28, msimu ujao. Mchezaji huyo alicheza kwa mkopo Juventus msimu uliopita (Mail)

Kiungo wa QPR Sandro ameshindwa kupita katika vipimo vya afya ili kujiunga na Sporting Lisbon, baada ya kukubaliana mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Ureno (Independent)

Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli anakaribia kujiunga na Besitkas ya Uturuki, kwa mujibu wa wakala wake (Spox.com)

Kiungo wa Valencia Andre Gomes, 22, huenda akahamia Manchester United (Mundo Deportivo)

Leicester City wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo Nampalys Mendy, 23, kutoka Nice (Mirror)

Manchester City wanataka kuwazidi kete Manchester United kumsajili winga wa chalke, Leroy Sane, 20, ambaye thamani yake ni pauni milioni 40 (Suddeutsche Zeitung)

Manchester United pia wanamfuatilia mshambuliaji wa Basel, Breel Embolo, 19 (Bild)

Beki wa Sunderland Santiago Vergini, 27, huenda akasajiliwa na Boca Juniors ya Argentina (Sunderland Echo)

Wakala wa kiungo wa Newcastle, Giorginio Wijnaldum, 25, anasema hakuna hatua zozote zilizopigwa kuhusu mchezaji huyo kuhamia Roma (Chronicle)

Swansea City watazungumza na Nathan Dyer, 28, kuona kama ataendelea kusalia katika klabu hiyo aliyoichezea kwa mkopo akitokea Leicester (South Wales Evening Post)

Kiungo wa Ufaransa Clement Chantome, 28, yuko katika mazungumzo ya kina na timu mbili za EPL kwa uhamisho wa bure, baada ya kukataa mkataba mpya Bordeaux (Sunderland Echo).

Didier Kavumbagu Aikacha Mbeya city, Atimkia Mashariki Ya Mbali
Young Africans Kufanya Usajili Wa Kufuru