Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Kahama Mjini iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, James Lembeli dhidi ya Jumanne Kishimba ambaye ni mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, imeshindwa kuendelea kusikilizwa leo.

Kesi hiyo namba 1 ya Uchaguzi ya mwaka 2015 iliyoanza kusikilizwa mahakamani hapo jana imeshindwa kuendelea baada ya upande wa utetezi kuwasilisha hati ya pingamizi ikiutaka upande wa mlalamikaji kuondoa kifungu cha 8 katika hati yake chenye kipengele a, b, na c.

Upande wa utetezi uliieleza mahakama kuwa kifungu hicho kinacholalamikia matumizi ya rushwa katika zoezi la uchaguzi wa mbunge wa jimbo hilo hakiko sawa kisheria.

“Hoja ya kwetu kama alivyofafanua wakili iko wazi kabisa. Kwahiyo mimi nina imani na mahakama, kama ambavyo upande wa pili nao una imani na mahakama. Tuipe mahakama nafasi ya kuweza kufanya uamuzi,” alisema Lembeli.

Mahakama hiyo itatoa uamuzi wa pingamizi hilo Januari 8 mwaka huu, na kuwezesha kesi ya msingi kuendelea kusikilizwa.

 

 

Justin Bieber aeleza Kwanini Hataweza tena kuwa na Selena Gomez
Facebook Wamkatalia Mbunge Kupost Picha hii