Rais wa Tanzania, Dkt. John Mgufuli amezungumza kwa njia yasimu na Rais Mteule wa Burundi, Evariste Ndayishimiye ambapo amempongeza kufuatia Mahakama ya katiba nchini humo kuagiza rais huyo aapishwe haraka.

Kwa mujibu wa taaarifa iliyotolewa imeeleza kuwa Rais Magufuli amemuhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza kukuza ushirikiano na Burundi ambapo amempa pole Rais huyo mteule kwa msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza aliyefariki dunia Juni 9, 2020.

Aidha Rais Magufuli amemuomba kufikisha salamu za rambirambi kwa warundi wote na kuwasihi waendelee kuwa watulivu na wastahimilivu, na watanzania wote wanaungana na warundi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Taharuki: Wimbi la pili maambukizi ya Corona China laibuka
Burundi: Mahakama ya yaagiza kuapishwa kwa rais mteule mapema