Ndoto za beki wa kulia kutoka nchini Hispania Hector Bellerin za kuendelea kubaki kaskazini mwa jijini London zimetimia, baada ya kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 21, ameripotiwa kusaini mkataba wa muda mrefu, jambo ambalo linachukuliwa kama sehemu ya kuendeleza uwajibikaji wake, kwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha The Gunners.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, aliwathibitishia waandishi wa habari majuma kadhaa yaliyopita, kuhusu uhakika wa beki huyo kusalia katika himat ya yake, kutokana na tetesi zilizokua zimechukua nafasi kubwa mitandaoni kuhusu mustakabali wa Bellerin.

Wenger alidiriki kuweka wazi mkakati wa mazungumzo yaliyokua yakiendelea kati yake na Bellerin, kufuatia uwepo wa taarifa za FC Barcelona ambayo ilimkuza mchezaji huyo, kutaka kumrejesha Camp Nou.

Bellerin alisajiliwa na Arsenal mwaka 2011 kama sehemu ya makubaliano ya kuuzwa kwa kiungo Cesc Fabregas aliyetimkia FCBarcelona kwa wakati huo.

40 Kuunda Kikosi Bora Cha Mwaka 2016
Jurgen Klinsmann Afungasha Virago