Mlinda mlango kutoka nchini England Joe Hart, amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Torino kwa mkopo akitokea Man City.

Hart alilazimika kuondoka jana kwenye kambi ya timu ya taifa ya England kwa ndege binafsi na kuelekea mjini Turin, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya pamoja na kusaini mkataba wa mkopo wa muda mrefu.

Nyaraka za mchezaji huyo kati ya klabu za Man City na Torino zilikamilishwa usiku wa kuamkia hii leo, ikiwa ni muda sahihi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa hii leo.

Klabu ya Torino imekubali kulipa sehemu ya mshahara wa Joe Hart ambayo inakaribia kiasi cha Pauni elfu 55, na Man City itachangia Pauni laki moja na elfu thelathini zilizosalia kwa juma.

Jukwaa la wahariri lapinga kufungiwa Radio 5, Magic Fm
Chelsea Waushtua Ulimwengu Wa Soka