Mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid imetangaza kumsajili mshambuliaji Mariano Díaz Mejía, akitokea Olympique Lyonnais  ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitano.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, anarejea Santiago Bernabeu baada ya mwaka mmoja, ulioshuhudia akiondoka chini ya utawala wa meneja Zinedine Zidane, kufuatia kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Mariano anatarajiwa kutangazwa rasmi katika mkutano na waandishi wa habari kesho Ijumaa, na shughuli hiyo itafanywa na Rais wa klabu Florentino Perez.

Mshambuliaji huyo wa Jamuhuri ya Dominican, alikuzwa na kituo cha kulea na kuendeleza vipaji kwa vijana cha Real Madrid, na alitumika kama mchezaji wa akiba katika michezo minane mwaka 2017, kabla ya kutimkia Olympique Lyonnais, ambapo amecheza michezo 30 ya ligi daraja la kwanza nchini humo (Ligue 1) msimu uliopita, na kufunga mabao 18.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Olympique Lyonnais, imeleza kuwa Mariano ameondoka klabuni hapo kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 33, ikiwapa ni faida ya Euro milioni 25, baada ya kumsajili kwa Euro milioni 8 akitokea Real Madrid mwaka 2017.

Siphiwe Tshabalala ajiunga na BB Erzurumspor ya Uturuki
DC Kasesela atembelea kijiji ambacho hakijatembelewa na DC tangu 2010