Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Timu ya Yanga imepanga kwenda kuweka kambi yake Pemba, Zanzibar kujiandaa na mechi ya ngao ya Jamii watakayocheza dhidi ya watani wao wa jadi Simba.
 
Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Aidha, Kambi hiyo itakuwa ya pili kwa Yanga kutoka nje ya Jiji la Dar es Salaam baada ya hivi karibuni kurejea kutoka mkoani Morogoro ambako walikaa kwa wiki mbili.
 
“Tutaondoka Dar Jumapili asubuhi kuelekea Unguja, hapo tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege, usiku wa siku hiyo hiyo, baada ya hapo Jumatatu tutaondoka kwenda Pemba,” amesema Mkwasa
 
  • Yanga kupimana ubavu na Ruvu Shooting
 
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kuwa wameichagua Pemba kutokana na utulivu uliopo kisiwani hapo ambao utampa nafasi nzuri Kocha wa Klabu hiyo,
George Lwandamina kupata nafasi ya kukiandaa kikosi hicho vizuri.
 
  • Wagombea Sita Wa Urais TFF Uso Kwa Uso Kwenye Kipindi Maalum
 
Hata hivyo, ameongeza kuwa, maandalizi ya kambi hiyo tayari yamekamilika na wametuma watu kwa ajili ya kuandaa kambi hiyo itakapofikia timu yao

Maximo Amfanyia Kampeni Mwakalebela
Korea Kaskazini: CIA wamepanga kumuua Kim Jong-un