Klabu ya Young Africans ya Jangwani jijini Dar es Salaam leo itatupa karata yake ikiwa nyumbani katika uwanja wa Uhuru dhidi ya Ndanda FC wana Mtwara Kuchele katika mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Ni kazi kwa wana Jangwani kuamua kumsogelea kileleni mtani wao wa Jadi Simba SC ambaye amewazidi pointi 4 muhimu akiwa na pointi 41 kati ya michezo yake 17, dhidi ya Mabingwa hao wa mara mbili mfululizo wenye pointi 37.

Yanga inaingia uwanjani leo baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wana African Lyon katika mchezo wao wa Ijumaa iliyopita. Hata hivyo, endapo watashinda bado watakuwa wamemsogelea tu mnyama Simba kileleni wakimuachia hatua moja mbele ya pointi 1 atakayofunga nayo mwaka.

Kocha George Lwandamina ameonesha kuichukulia kwa uzito unaofaa mchezo wa leo kwa kuyatanguliza majembe yake yote huku akifanya mabadiliko ya kumuanzisha kinda Emmanuel Martin aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka JKU ya Zanzibar mwezi huu.

Winga huyo wa atamuweka benchi Deus Kaseke, na hii inatokana na namna alivyoweza kumkuna kichwa Lwandamina katika mechi dhidi ya African Lyon akiingia kutoka benchi.

Wasaka magoli Donald Ngoma (Mzibabwe) na Amissi Tambwe (Mrundi) wote watafanya msako wa pointi tatu muhimu kwa timu hiyo leo.

Katika mzunguko wa kwanza, Yanga ilitoshana nguvu na Ndanda kwa sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara wakati Yanga ikiwa chini ya Mholanzi Hans Van Pluijm.

Hiki ni kikosi kizima cha Yanga leo:

Deo Munishi ‘Dida’,

Juma Abdul,

Mwinyi Hajji Mngwali,

Vincent Bossou

Kevin Yondan

Said Juma ‘Makapu’

Simon Msuva

Haruna Niyonzima

Donald Ngoma

Amissi Tambwe

Emmanuel Martin.

Benchi: Ally Mustafa ‘Barthez’, Andrew Vincent ‘Dante’, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa, Geoffrey Mwashuiya na Deus Kaseke.

Video: Zantel yatii agizo la Hapi, yalipa deni lililodumu miaka 7
Wafugaji watishia kuchukua maamuzi magumu