Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara Klabu ya Yanga inatarajia kushuka dimbani jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kumenyana na Ruvu shooting katika mchezo wa kirafiki.

Akizungumza na Dar24 media Afisa habari wa timu hiyo, Dismas Ten amesema kuwa wanatarajia kushuka dimbani jumamosi hii kumenyana na Ruvu Shooting katika mchezo wa wa kupimana nguvu.

’’Tunatarajia kushuka dimbani jumamosi hii kucheza na Ruvu shooting katika mchezo wa kujipima uwezo na kwa upande wa maandalizi kikosi chanyewe kiko vizuri hivyo wapenzi na mashabiki wa Yanga watarajie matokeo mazuri,’’amesema Dismas

Aidha, ametoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenda kushuhudia mchezo wao huo wa kirafiki ikiwa ni mchezo wao wa pili baada ya kucheza na Singida United na kuibuka kwa ushindi wa 3-2.

Hata hivyo,  Yanga inaingia dimbani huku ikiwa katika muendelezo wa maandalizi ya mchezo wa ngao ya hisani utakaopigwa Agost 23 mwaka huu dhidi ya watani wao wa jadi Simba Sports Club.

Wagombea Sita Wa Urais TFF Uso Kwa Uso Kwenye Kipindi Maalum
Serikali kuwadhibiti wasafirishaji fedha nje ya nchi