Mabingwa wa soka nchini timu ya Yanga, wamethibitisha kuwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya uko kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara leo dhidi ya wenyeji Mbeya City.

Yanga kupitia taarifa yake imesema imejiridhisha na maandalizi ya uwanja huo ambao utatumika kwenye mchezo wa leo na tayari maandalizi ya uwanja yamekamilika kwa ajili ya mchezo  wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City.

Aidha, Yanga tayari ipo jijini Mbeya ambako imetua jana jioni kwa ndege, ikiunganisha baada ya siku moja tu kutoka nchini Ethiopia ambako ilicheza mchezo wake wa mtoano na kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho siku ya Jumanne.

Yanga leo itacheza mchezo wake wa raundi ya 23, ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na alama 47 nyuma ya Simba yenye alama 59 kileleni ikiwa imecheza mechi 25.

Hata hivyo, Kwa upande wao Mbeya City wao watakuwa wanacheza mchezo wa raundi ya 25, wakiwa na alama 26 katika nafasi ya 11. Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya 10:00 jioni.

 

Picha: Mwili wa Masogange ukitolewa Muhimbili na kupelekwa Leaders kwa kuagwa
Iran yasema iko tayari kuendelea na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Comments

comments