Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga watashuka dimbani kuwavaa maafande wa JKT Mlale siku ya Jumatano katika pambano la hatua ya 16 ya Kombe la Shirikisho.

Awali mechi hio ilipangwa kuchezwa Machi 1 lakini Yanga waliomba ichezwe Jumatano ili kupata muda zaidi wa kujiandaa na hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Maafande wa JKT Mlale wanaoshiriki ligi daraja la kwanza walifanikiwa kuingia hatua ya 16 bora baada ya kuwatoa timu ya Majimaji katika hatua ya 32 iliyochezwa mwezi uliopita.

Katika mechi nyingine za hatua ya 16 Bora, Azam watakuwa wageni wa Panone ya Daraja la kwanza mjini Moshi, Simba wataawalika Singida United iliyopanda Daraja la Kwanza.

Coastal Union itapambana na Mtibwa Sugar,  Ndanda na JKT Ruvu wakati Mbeya City na Prisons zitaendeleza upinzani wao wa jijini Mbeya.

Timu ya Geita Gold ambayo inasubiri hatma yake ya kupanda ligi Kuu msimu ujao itasafiri hadi Mwanza kumenyana na Toto Africans huku Mwadui ikiialika Rhino Rangers.

Pluijm: Bado Mapema Sana Kuitangazia Ubingwa Yanga
Kifaru: Mtibwa Imepoteza Kwa Kuwakosa Wachezaji Wake Muhimu