klabu ya Yanga imesema kuwa inasubiri dakika 90 tu za mchezo wao uwanjani ili kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya watani zao klabu ya Simba.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten ambapo amesema kuwa maandaalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia 100.

“Mazoezi ya siku nane yamefanyika kwa umakini mkubwa  kwa upande wa timu na kwa upande wa uongozi maanadalizi yote muhimu yamekwisha fanyika na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za uwanjani. Hali ya wachezaji ipo vizuri kabisa kasoro Ngoma pekee bado yuko nje ya kikosi kwa majeraha. Suala la nani ataanza au kutocheza tumewaachia benchi la ufundi kuona nani wanaweza kumtumia kulingana na ‘game plan’ waliyokuwa nayo,”amesema Ten

Hata hivyo, kwa upande wake Kocha, Zahera Mwinyi amesema kuwa ameridhishwa na uwezo wa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Yanga, anachohitaji ni muda wa kukaa nao ili aendelee kuwajenga na kuwaimarisha zaidi tayari kwa michezo ya kimataifa.

Serikali kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto
Kilimo cha Bangi chahalalishwa kisheria