Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza rasmi visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya tarehe 02/01/2016 kati ya JKU na URA muda wa saa 10:15 jioni na saa 2:15 usiku watacheza kati ya Simba ambae ndie bingwa mtetezi dhidi ya Jamhuri kutoka Wete Kisiwani Pemba michezo yote itasukumwa kwenye dimba la Amaan.

Katika mashindano hayo yamejumuisha timu nane, tatu kutoka Visiwani Zanzibar ambao ni JKU, Mafunzo na Jamhuri ambapo pia timu 4 kutoka Tanzania bara zikijumuishwa Simba (Bingwa mtetezi), Yanga, Azam, na Mtibwa Sugar na timu kutoka nje ya Tanzania ni moja tu ambayo ni URA ya Uganda.

Timu hizo 8 zimegawanywa kwenye makundi mawili “A” na “B” kwa kila moja timu 4.

Kundi “A” kuna timu ya Simba, Jamhuri, JKU na URA, wakati kundi “B” kuna timu ya Yanga, Mafunzo, Azam na Mtibwa Sugar.

Timu 2 bora kwa kila kundi zinatarajiwa kutinga nusu fainali na zitakozofanikiwa kuingia fainali zitacheza fainali tarehe 13/01/2016 saa 2:15 kwenye dimba la Amaan.

Ufisadi wa Mabilioni waibuliwa tena Bandarini, Maelfu ya Makontena Na Magari Yavushwa
Van Gaal Aahirisha Kujiuzulu Man Utd