Klabu ya soka ya Yanga hii leo imeendele na mazoezi yake katika uwanja wa karume jijini Dar es Salaam kujiaandaa na mchezo wao wa kesho wa kombe la FA dhidi ya JKT Mlale.

Yanga wameendelea na mazoezi yao baada ya kutoka katika mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya watani zao klabu ya soka ya simba.

Katika mchezo huo ulioibua hisia nyingi za mashabiki wa soka klabu ya Yanga iliibuka kidedea kwa kuwatandika watani zao hao mabao 2-0 ikiwa ni rekodi inayofanana na mzunguko wa kwanza walipokutana katika uwanja huo huo na Yanga kuibuka na ushindi kama huo.

Yanga inacheza mchezo wake kesho wa kombe la FA huku ikiwa na michezo miwili migumu mbeleni dhidi ya wapinzani wao wakubwa siku ya jumamosi klabu ya Azam FC na mchezo wa marudiano kombe la vilabu bingwa Afrika dhidi ya Cercle De Joachim ya Mauritius mwezi march mwaka huu.

Twiga Stars Waendelea Kuwavutia Kasi Zimbabwe
TFF, KTA Zazindua Programu Ya Maendeleo Ya Soka Kwa Wanawake