Timu ya Yanga kupitia Katibu wake Jonas Tiboroha amesema kuwa uongozi wa timu hiyo utamchukuliwa hatua za kinidhamu mshambuliaji wa timu hiyo Haruna Niyonzima kwa tabia yake kuchelewa kujiunga na timu hiyo pindi anapopewa ruhusa ya kuihudumia timu yake ya taifa kitendo kinachoigharimu timu.

Amesema mchezaji huyo amekuwa akifanya kosa hilo mara kwa mara na kuigharimu timu hiyo wakakti akijua yeye ni mchezaji tegemezi katika timu hiyo kwa wakati huu.

“Kinachosikitisha zaidi amezima simu zake zote kiasi kwamba sisi hatujui yuko wapi. Wakati alipokuwa Ethiopia, alikuwa anawasiliana na kocha (Hans van der Pluijm) na alijua umuhimu wa kuwahi, sasa kitendo hiki tukitafsiri vipi?”amehoji Tiboroha.

Mnyika Adai Tamisemi Kuamishiwa Ofisi Ya Rais Ni Mbinu Dhidi Ya Wapinzani
Yaya Toure: Soka Haikua Ndoto Yangu