Baada ya taarifa za ujio wa kocha mpya Mzambia George Lwandamina na kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha wa timu Hans Van der Pluijm, Yanga imeendelea kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi na kumleta mtendaji mkuu mpya Jerome Dufourg kutoka nchini Ufaransa, ambaye amaesaini mkataba wa miaka mitatu.

Dufourg ambaye vile vile amewahi kufanya kazi katika Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na klabu ya FC Talanta inashiriki Ligi Daraja la pili nchini Kenya anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam wakati wowote kuanzia leo kuanza kazi rasmi.

Dufourg anasifika kwa utendaji ulio bora katika sehemu zote alizopita na jukumu lake kubwa litakuwa ni kuhakikisha timu inakuwa na uwezo wa kujiendesha yenye kwa maana ya mapato ya klabu yazidi matumizi.

Vigogo watatu bandari kortini kwa rushwa
Asilimia 90 ya maoni muswada wa habari yafanyiwa kazi