Klabu ya Yanga imekabidhi rasmi ubingwa kwa watani wao wa Jadi, Simba SC baada ya kuchapwa bao 2-0 na wenyeji wao Tanzania Prisons ‘wajela jela’ katika mchezo uliochezwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya jioni ya leo Mei 10, 2018.

Bao la kwanza la wajela jela limepatikana katika dakika ya 58 kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Eliuter Mpepo baada ya mchezaji wa Yanga Thaban Kamusoko kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Aidha, dakika ya 83 ya mchezo huo Tanzania Prisons walipata bao la pili kupitia Juma Abdul krosi iliyotengenezwa na Mohamed Rashid baada ya vuta ni kuvute na walinzi wa lango la Yanga.

Kutokana na ushindi huo wa Tanzania Prisons wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, matokeo hayo yanaipa rasmi Simba SC ubingwa wa moja kwa moja wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/ 2018 na kuifanya timu hiyo kunyakua kikombe hicho mara ya 19 na mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni mwaka 2012.

Video: Wanaotaka kujua zinapokwenda fedha za serikali wanitafute- Makonda
Kuteuliwa sio tatizo, ukishindwa tunakurudisha- JPM