Kikosi cha timu ya Yanga kimepokea kitita cha milioni 10 kutoka kwa wadhamini wao, kampuni ya GSM ikiwa ni sehemu ya kuwapa motisha baada ya kuifunga Ndanda FC kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona,

Patrick Sibomana ndiye aliibuka shujaa kwa kufunga bao moja la ushindi kwa Yanga dhidi ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi Kuu huku Yanga ikiwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa na msaidizi wake Said Maulid baada ya kumtimua Mwinyi Zahera.

Yanga iliwalazimu wasubiri mpaka dakika ya 75 kushinda mchezo huo mara baada ya Sibomana kupachika bao hilo kwa mpira wa adhabu akiwa nje kidogo ya 18 ambao ulizama jumla ndani ya nyavu za lango la Ndanda FC.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 10 ikiwa imecheza mechi tano imeshinda mbili na imetoa sare tatu na kupoteza mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting.

Kabla ya Mechi hiyo, GSM ilitoa ahadi ya kuipa Yanga Tsh milioni 10 endapo itashinda mechi hiyo iliyochezeka jana na wanakuchere  jambo ambalo Yanga wamelitekeleza.

John Cena amfanyia suprize  ya aina yake Madjozi
Jafo asema uchaguzi upo palepale

Comments

comments