Hatimaye jua limewaka na mashabiki wa Yanga wameiona siku waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu huku wakipata mtihani wa kuhesabu saa kwa kiu ya kuyapata majibu yaliyojificha wakati timu hiyo itakapoivaa Al Ahly majira ya saa 1 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki, mjini Alexandria nchini Misri.

Pambano hilo la marudioano katika hatua ya 16 Bora litashuhudiwa katika uwanja wa Jeshi wa Borg El Arab ambapo Yanga wakiwa ugenini watalazimika kupata ushindi ili waweze kusonga mbele au kupata sare ya magoli kuanzia 2-2 kwakuwa katika awamu ya kwanza ya mchezo kati yao walipata sare ya 1-1 wakia nyumbani jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Klabu hiyo ya Jangwani, Jerry Muro amesema kuwa timu hiyo iko fiti kuwakabiri Al Ahly ikiongozwa na Kocha Hans van der Pluijm.

Endapo timu hizo zitatoka sare ya 1-1 zitalazimika kumtafuta mshindi kwa njia ya matuta.

Hospitali yageuka duka la watoto, yauza vichanga kwa bei hii
Fidel Castro ajitabiria kifo, atoa hotuba yake nzito