Klabu ya Yanga imekanusha taarifa zilizogaa mitandaoni kuhusu kujiuzuru kwa Mwenyekiti wao, Yusuph Manji na kusema kuwa taarifa hizo si za kweli na wanachama wote wanatakiwa kuzipuuza.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Charles Mkwasa ambapo amesema kuwa hajapata taarifa rasmi juu ya ukweli wa suala hilo lakini amethibitisha kuwa bado hajawasiliana na Manji kama kweli amechukua uamuzi huo.

“Sijapata taarifa hizo rasmi, mimi ndiyo mtendaji mkuu wa klabu, bado sijakabidhiwa barua kwa kuwa sifanyi kazi kwa kutumia mitandao, tunajua kuwa mitandaoni kuna taarifa nyingi ambazo siyo za kweli na zipo nyingine ambazo zimesababisha baadhi ya wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, hivyo nasubiri kuona kama ni kweli, basi nitapatiwa barua rasmi na nitatoa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo.”amesema Mkwasa.

Hata hivyo, mapema hii leo kumekuwa na taarifa inayosambaa mitandaoni ya kujiuzuru kwa Manji huku ikiwa imesainiwa na Mwenyekiti huyo akieleza uamuzi wake wa kutangaza kujiuzuru.

Griezman kung'oka Atletico Madrid
?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 23, 2017