Kundi moja la wawekezaji linaloungwa mkono na serikali ya China linataka kuinunua Liverpool kwa pauni milioni 700 (Independent).

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Spain, Nolito, 29, ambaye ana kipengele cha uhamisho cha pauni milioni 14 kwenye mkataba wake na klabu ya Celta Vigo (Sun)

Everton wanajiandaa kumpa mkataba mnono Romelu Lukaku, 23, wenye mshahara wa zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ananyatiwa na Chelsea na Juventus (Daily Mail)

Everton wanafikiria kumsajili kiungo wa Roma, Kevin Strootman, 26, baada ya meneja mpya Ronald Koeman kupewa pauni milioni 100 za kununua wachezaji (Liverpool Echo)

Stoke wameanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, kwa pauni milioni 15. Usajili wa mchezaji huyo mwenye asili ya Burundi ni kipaumbele cha juu cha meneja Mark Hughes (Guardian)

Mabingwa wa EPL Leicester wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo Nampalys Mendy, 23, kutoka Nancy kwa pauni milioni 9.5 (Le 10 Sport),

Chelsea huenda wakalazimika kutoa pauni milioni 50 iwapo wanataka kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci, 29 (Gazzetta dello Sport).

Chelsea pia wameambiwa na Valencia kuwa lazima watoe pauni milioni 42 kama wanamtaka kiungo Andre Gomes, 22 (Daily Mirror).

Chelsea vilevile wanazungumza na kipa wa Marseille Steve Mendanda, 31, ambaye mkataba wake unamalizika mwezi ujao (Evening Standard), wakati huohuo mshambuliaji wa Chelsea, Pedro, 28, amezungumza na rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu kuhusu kurejea Camp Nou (Bein Sports).

Borussia Dortmund wamezuia uhamisho wa kiungo Henrikh Mkhitaryan kwenda Mancheser United. Mchezaji huyo kutoka Armenia amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake (Times), Arsenal ndio timu pekee iliyopanda dau kumtaka Mkhitaryan, lakini mchezaji huyo angependa kwenda Old Trafford (Squawka).

Tottenham wameambiwa watoe pauni milioni 12 iwapo wanataka kumsajili kiungo kutoka Croatia, Milan Bade, 27 kutoka Fiorentina (Daily Express).

Kiungo wa Sunderland Emanuele Giaccherini, 31, angependa kuhamia Fiorentina, kwa mujibu wa wakala wake (Radio Blu).

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 33, atamalizia mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake Etihad, wa pauni 220,000 kwa wiki, baada ya kukataa kuhamia Italia na China (Daily Mirror)

West Brom wanamtaka kiungo kutoka Ufaransa, Moussa Sissoko, 26, ambaye anataka kuondoka Newcastle baada ya timu hiyo kushuka daraja. Newcastle wanataka pauni milioni 15 kumuuza (Chronicle)

Kiungo kutoka Uganda Khalid Aucho, 22, amesema anakaribia kujiunga na Rangers ya Scotland, akitokea Gor Mahia ya Kenya (Goal).

Picha: Roberto Di Matteo Atambulishwa Rasmi
Mashabiki Wamnanga Anthony Martial Katika Mtandao Wa Twitter