Ronald Koeman hatimaye anatarajiwa kuthibitishwa kuwa meneja mpya wa Everton siku ya Jumanne (Daily Mail)

Winga kutoka Ujerumani Leroy Sane, anatarajiwa kujiunga na Manchester City akitokea Schalke baada ya michuano ya Euro 2016 (Sport).

Borussia Dortmund watawaambia Manchester City kutopanda dau la kumtaka kiungo Oleksandr Zinchenko, iwapo wanataka kumsajili Pierre Emerick Aubameyang. City wanafanya mazungumzo na Dortmund kumsajili Aubameyang, lakini klabu hiyo ya Ujerumani haiko tayari kuzungumza na City iwapo watamtaka Zinchenko pia (Sun).
Beki kutoka Ufaransa Aymeric Laporte, 22, amekataa nafasi ya kujiunga na Manchester City na badala yake amesaini mkataba mpya Athletic Bilbao (Daily Mail).

West Ham wamewaambia Chelsea kuwa hawatomuuza kiungo wao Dimitri Payet, 29, kwa bei yoyote ile (Daily Mirror).

Napoli watampa mkataba mpya mshambuliaji wao Gonzalo Higuain na mshahara wa pauni 110,000 kwa wiki. Mshambuliaji huyo amehusishwa na kwenda Liverpool (Rai Sport).

Winga wa Leicester Riyad Mahrez, 25, amepewa mkataba mpya na mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki, ikiwa ni jitihada za mabingwa hao kumshawishi asiondoke (Daily Telegraph).

Chelsea wamemuulizia beki wa Lyon, Samuel Umtiti, 22 (Mundo Deportivo).

West Ham watamsajili winga wa Valencia, Sofiane Feghouli, 26, bila malipo yoyote (L’Equipe).

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili beki wa Manchester United, Matteo Darmian, 26 (Bleacher Report).

Borussia Dortmund huenda wakaamua kumuuza Hendrikh Mkhitaryan mwishoni mwa wki, huku Arsenal wakiwa miongoni mwa timu zinazotaka kumsajili mshambuliaji huyo kutoka Armenia (London Evening Standard).

Usajili mpya wa Manchester City Ilkay Gundogan, 25, anatarajiwa kupona jeraha lake mwishoni mwa mwezi Agosti, au mwanzoni mwa Septemba (Manchester Evening News)

Kiungo kutoka Ureno Joao Carlos Teixeira, 23, amesema anaondoka Liverpool kwenda kutimiza ndoto zake Porto (Liverpool Echo).

Shilole ameshindwa kuivumilia ‘Jike Shupa’ ya Nuh Mziwanda, 'Umemiss mkong'oto??'
Hizi Hapa Sababu Za Kufutwa Kwa Umitashumta Na Umisseta