Beki wa pembeni Yassin Mustafa huenda akatimka Young Africans na kujiunga na klabu moja wapo itakayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23.

Yassin anahusishwa kuwindwa na klabu za Polisi Tanzania, Ihefu FC, Dodoma Jiji FC na Singida Big Stars (SBS), katika kipindi hiki cha Dirisha la Usajili kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Beki huyo aliyejiunga na Young Africans misimu miwili iliyopita akitokea Polisi Tanzania, anapewa nafasi kubwa ya kuondoka Jangwani, kufuatia kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Licha ya kuwa FIT nafasi ya Beki wa Kushoto Young Africans, imekua ikijazwa na Farid Musa na Kibwana Shomary ambao kiasili sio wachezaji wanaocheza nafasi hiyo.

Kwa mtazamo huo Yassin ataendelea kuwa na wakati mgumu wa kucheza kikosi cha kwanza cha Young Africans msimu ujao, hivyo ameanza kusaka namna ya kuondoka ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara na katika kikosi cha kwanza.

Mchezaji mwingine anayepewa nafasi kubwa ya kuondoka Young Africans anayecheza nafasi ya Beki wa Kushoto ni David Bryson, aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita 2021/22 akitokea KMC FC.

Simba SC yakaa mguu sawa
Jemedari Said akoleza vita na Haji Manara