Baada ya kuondoka katika klabu ya Manchester City, Yaya Toure ameibuka na kumtuhumu kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola kuwa na matatizo na wachezaji wakiafrika.

Tangu ujio wa Pep Guardiola katika klabu ya Man City, Toure alianzishwa mechi 22 tu msimu wa 2016-2017 na akaambiwa abaki katika klabu hiyo kwa mwaka mwengine mmoja, lakini amecheza michezo 17 tu msimu uliomalizika mara zote akitokea benchi isipokuwa katika mchezo dhidi ya Brighton ambapo alicheza dakika 86.

Toure anaamini kwamba sababu ya yeye kutochezeshwa sio umri wake bali ni kwa sababu yeye ni mweusi, ”Alinionyesha ukatili, nilijiuliza iwapo ni kwa sababu ya rangi yangu. Mimi sio wa kwanza kuzungumza kuhusu tofauti ya tunavyochukuliwa, pengine sisi waafrika hatuchukuliwi kama wengine wanavyochukuliwa”, alisema Toure.

Akizungumza na kituo cha habari za michezo nchini Ufaransa Toure aliongeza kuwa anataka kuwa mchezaji ambaye atavunja mtazamo wa Guardiola kwani amegundua kuwa Pep ana matatizo na wachezaji wa Afrika kila anapokwenda.

Kiungo huyo wa kati wa timu ya taifa ya Ivory Coast alicheza katika klabu ya Barcelona kwa misimu miwili chini ya usimamizi wa Guardiola kabla ya kusajiliwa na klabu ya City kwa dau la paundi milioni 24 mwaka 2010.

 

Jordan Pickford akabidhiwa gwanda England
Aswekwa rumande kwa kumdanganya kiongozi wa mbio za Mwenge