Kila mtu ana kipaji chake katika maisha na ni wachache ambao huvilinda vipaji vyao hadi ukubwani kwani wapo waliotamani kufanya hivi lakini mwisho wa siku wakajikuta wanafanya kitu kingine kabisa ambacho hawakudhamiria kufanya.

Kwa mchezaji wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, akiwa mdogo amedai kuwa alipenda sana mchezo wa karate kabla ya kuhamia kwenye soka.

Karate ndio mchezo ambao kiungo huyo alikuwa ameanza kucheza wakati akiwa bado mdogo na huenda mpaka sasa angebaki kwenye mchezo huo endapo baba yake mzazi asingemkataza akihofia angepata majeraha kupitia mchezo huo.

Inadaiwa kuwa akiwa mdogo katika kipindi cha wiki moja, aliweza kufanya vyema na kuteuliwa kushiriki katika mashindano makubwa yaliyofanyika Kenya, ambayo hata hivyo hakwenda kutokana na baba yake kumzuia.

Kiungo huyo amekuwa na mafanikio makubwa kupitia soka na juzi alifanikiwa kushinda tuzo ya BBC ambayo hutolewa kila mwaka kwa mchezaji bora Afrika.

Yanga Wapandwa Hasira Dhidi Ya Niyonzima
Dylan Kerr Amfungulia Milango Hassan Kessy