Jaji wa Los Angeles huko Nchini Marekani ameamua kuridhia na kukubali ombi la rapa Kanye west kubadili rasmi jina lake, hivyo kuanzia sasa msanii huyo atatambulika kwa jina la ‘YE’ bila ya kuwa na jina la kati wala la mwisho kama ilivyo kawaida ya mfumo wa majina Duniani kote.

Kanye West atajulikana kisheria kama “Ye,” kwa matakwa ya rapa huyo, jaji wa Los Angeles alitoa uamuzi wa kuridhia Ombi hilo siku ya Jumatatu.

Mapema Agosti 24,2021 Kanye West aliwasilisha ombi la kubadilisha jina lake kutoka kuitwa Kanye West hadi kuitwa ‘YE’, akihitaji jina hilo litambulike rasmi kisheria huku akidai alikuwa akifanya mabadiliko hayo kwa sababu binafsi. Swala la kubadili rasmi jina lake linaibua maswali ya ni kwa namna gani hatua hiyo itaathiri shughuli za kibiashara za rapa huyo mwenye umri wa miaka 44.

YE mwenyewe amewahi kuvitaja miongoni mwa vyanzo vilivyompekea kuchukua hatua za kubadilisha jina lake hata alipofanya mahojiano maalumu na mtangazaji Big Boy wa Redio Real923la mwaka 2018, ambapo moja ya sababu alizotaja Kanye ni jina hilo kuwa moja ya majina yaliyotajwa sana kwenye kitabu cha Biblia.

Kwa sasa unaruhusiwa kufuta kabisa jina Kanye West Kichwani kwako, tayari amelitupa kando na sasa anatambulika kisheria kama ‘YE’.

Korea kaskazini yarusha kombora tena
Ni wapi alipo  Papii Kocha?'