Watu 31 wameuawa kwenye mashambulizi ya anga yaliyoongozwa na Saudi Arabia siku ya Jumamosi.

Ofisi ya mratibu wa misaada ya kiutu ya Umoja wa Mataifa imesema watu wengine 12 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo yaliyolilenga eneo la Al Hayjah katika wiliya ya Maslub iliyo kwenye jimbo la Jawf kaskazini ya Yemen.

Grande amesema inashangaza kuwa hata baada ya miaka mitano ya mzozo wa Yemen pande zinazopigana zimeshindwa kuheshimu wajibu huo.

Yemen imetumbukia kwenye machafuko kati ya serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia na kundi la waasi wa Houthi lenye mafungamano na Iran tangu mwaka 2014.

Kibano chaja wanaouza nguzo za umeme
TMA yatahadharisha mvua za masika, wataja mikoa itakayoathirika zaidi

Comments

comments