Yemi Alade ameamua kuchukua hatua ya kiungwana na kuomba radhi baada ya kuandamwa kwenye mitandao kufuatia tweet yake inayoshambulia mastaa wa kike wa Nigeria kwa madai kuwa wanajiongezea makalio feki kwenye picha wanazoweka mtandaoni.

Shambulio hilo la Yemi lilionekana kumgusa moja kwa moja Tiwa Savage ambaye alijibu kwa maneno makali na baadaye timu yake ikaendelea na vita hiyo. Tiwa alimuonya Yemi kuwa asianzishe vita ambayo hawezi kuimaliza na kwamba yeye sio kama anayemfikiria.

“Usianzishe vita ambayo huwezi kuimaliza. Niamini, mimi sio yule unayemfikiria. Niko kimya lakini usitake kunivuruga,” tafsiri isiyo rasmi ya tweet ya Tiwa.

Saa chache baadaye, Yemi Alade aliamua kuomba radhi akifafanua kuhusu tweet yake. Alieleza kuwa hakuwa na nia ya kuwachafua wanawake maarufu nchini humo, lakini alitaka kuwahamasisha kuacha kuchezea picha zao ili kujiongezea makalio ili kuwavutia mashabiki, na badala yake waamini kuwa wao ni wazuri tu kwa jinsi walivyo kiasili.

“Siko hapa kwa ajili ya kujitetea. Kama tweet yangu ya awali ilikuwa mbaya, naomba radhi kwa wanawake wenzangu na watu wote. Ninataka tujikubali hata kama sisi ni wadogo, wakubwa, wembamba, wanene, wafupi. Bila au tukiwa na makalio makubwa. SISI NI WAZURI,” aliandika.

Mjadala wa bifu kati ya wasanii hao wa kike umehamia kwa timu zao, ingawa wingi wa mashabiki wa Tiwa Savage unampa wakati mgumu Yemi Alade.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 24, 2018
Makomando wanaomlinda Waziri Mkuu waonesha uwezo