Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Yacouba Songne ameahidi kupambana katika michezo ya mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ili kuhakikisha anafunga mabao mengi kwa ajili ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora mwishoni mwa msimu .

Mshambuliaji huyo wa Young Africans anaipigia hesabu tuzo hiyo ya ufungaji bora, ambayo kwa msimu uliopita ilichukuliwa na mshambliaji kutoka nchini Rwanda na klabu ya Simba SC, Meddie Kagere aliyefunga mabao 22.

Hadi sasa Yacouba amefunga mabao manne katika michuano ya Ligi Kuu, huku akiachwa kwa tofauti ya mabao matano na Meddie Kagere anaeongoza orodha ya wafungaji bora msimu huu kwa kufikisha mabao tisa, akifuatiwa na mshambuliaji mwenzake wa Simba SC John Bocco mwenye mabao manane.

Mshambuliaji huyo amesema kutwaa tuzo ya ufungaji bora ni ndoto ya kila mshambuliaji, na kwa upande wake atajitahidi afunge zaidi kwa ajili ya kuichukua tuzo hiyo.

“Kila mshambuliaji ana ndoto na suala hilo hali ambayo ipo kwangu pia.“Nitakachofanya ni kufunga mabao mengi kwa ajili ya kujiweka katika orodha hiyo lakini pia kuisaidia timu iweze kufanya vizuri.

“Naamini Mungu atanisaidia katika suala hilo na mimi nitafanya vile ambavyo ninaweza,” alimaliza Yacouba.

Baraza la Seneti kuendelea na kesi ya Trump
PICHA: Patrick Aussems aanza kazi AFC Leopards