Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ Kelvin Yondani ataukosa mchezo dhidi ya Rwanda utakaofanyika kesho Jumamosi Desemba 9, 2017 kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos Kenya.

Yondani amepewa mapumziko ya siku tatu baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Zanzibar.

Hivyo atakosa mchezo huo wa kesho ukiwa ni miongoni mwa mechi mechi za michuano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki maarufu kama Cecafa Senior Challenge inayofanyika hapa Kenya.

Jopo la Madaktari wa Kilimanjaro Stars linaloundwa na Dk. Richard Yomba na Dk Gilbert Kigadye limethibitisha kuwa majeraha aliyoyapata Yondani sio makubwa na yanahitaji apumzike kwa saa 72 ambazo ni sawa na siku tatu.

Vipimo vilivyochukuliwa vinaonesha kuwa hakuna mfupa wowote ulioathirika zaidi ya kupata mshtuko kiasi kwa hiyo wamempa siku tatu za mapumziko wakiendelea kumtazama maendeleo yake kwa ukaribu.

Kwa upande wa Mbaraka Yusuph ambaye alipata majeraha ya misuli kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya, amepona na anatarajia kuingia kwenye program ya utimamu wa mwili.

Hata hivyo Mbaraka hataweza kucheza kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Rwanda.

 

Rekodi za muda wote za Tanzania bara Vs Zanzibar
Mudathir Yahya mchezaji bora Novemba