Kikosi cha Young Africans kinatarajia kuanza mazoezi yake leo (Mei 27, 2020) chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa. Mazoezi yatafanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam.

Mkwasa amesema atayatumia mazoezi ya leo kuangalia kama wachezaji walikuwa wanatekeleza program waliyopewa na kocha mkuu Luc Eymael.

“Wachezaji wote wako vizuri, tutaanza mazoezi rasmi kwa kuanza kutafuta basic endurance na ball work kidogo kwa sababu tumepata program ya kocha mkuu na tutaifanyia kazi.”

“Kwenye mazoezi kuna vitu lazima tuvizingatie (fitness, technic, tactic na phycology) naamini fitness itakuwepo lakini hatuwezi kuanza mazoezi kwa speed kubwa tutaanza taratibu.”

Jana wachezaji wote wa Young Africans walikutana na uongozi pamoja na jopo la madaktari kwa ajili ya kupimwa afya na kupewa taratibu za kujikinga dhidi ya Corona wakiwa mazoezini.

Australia yaanza jaribio la kwanza chanjo ya Corona
Watanzania 16 wakutwa na Corona Uganda