Klabu ya Young Africans imeahidi kumtangaza mchezaji wa kimataifa aliyesajiliwa klabuni hapo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo ambacho kitafungwa rasmi kesho Jumamosi (Januari 15).

Young Afruicans imetamba kumtangaza mchezji huyo, kupitia kwa Msemaji wao Haji Sunday Manara, alipozungumza na Waandishi wa Habari mjini Tanga mapema leo Ijumaa (Januari 14).

Manara amesema kabla ya Dirisha Dogo la Usajili halijafungwa kesho Jumamosi (Januari 15), klabu hiyo itamtangaza mchezaji wa kimataifa ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake.

Amewata Mashabiki na Wanachama wa Young Africans kuwa tayari kumpokea mchezaji huyo ambaye anaaminiwa ataongeza chachu ya kusaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

“Kabla Dirisha halijafungwa kesho Jumamosi, tutamtangaza mchezaji wa kimataifa, Mashabiki na Wanachama mjiandae kumpokea mchezaji huyo ambaye tunaamini ataongeza kitu kwenye kikosi chetu kinachowania ubingwa msimu huu kwa nguvu zote.” Amesema Manara. Katika kipindi cha Dirisha Dogo la usajili 2021/22, Young Africans tayari imeshawasajili wachezaji kadhaa akiwepo Denis Nkane, Aboutwalib Mshery, Crispin Ngushi, Salum Aboubakar ‘Sure Boy na Ibrahim Bacca.

Nandy aukana ujauzito
RASMI Chama arudi Simba SC