Kikosi cha Young Africans kimeondoka leo asubuhi kwa ndege kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City (M.C.C.).

Mchezo huo utachezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine na Young Africans pamoja na kuwa tayari imetwaa ubingwa, lakini  hawatakabidhiwa Kombe.

Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo amesema kwamba muda haukutosha kwa maandalizi ya Young Africans kutawazwa kesho.

“Ni jana ndiyo Yanga imekuwa bingwa, sasa kutoka muda ule jioni haikutosha kwa wadhamini (Vodacom) kujiandaa kwa sherehe za ubingwa. Hivyo, hilo halitafanyika kesho,”amesema.

Wambura amesema sasa Young Africans watakabidhiwa kombe lao katika mchezo dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda, Sijaona mjini Mtwara Mei 14, mwaka huu.

Yanga imejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Simba SC kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanamaanisha hakuna timu yoyote ya Ligi Kuu yenye uwezo wa kufikisha pointi 68 ambazo wanazo Yanga hadi sasa,  na bila ubishi timu hiyo ya Jangwani imetetea ubingwa.

Simba SC ina pointi 58 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kufikisha pointi 67 ikishinda michezo yake yote mitatu ilizobaki, wakati Azam FC inaweza kumaliza na pointi 66.

Danny Welbeck Amuweka Majaribuni Roy Hodgson
Lowassa anena tena jimboni kwake