Uongozi wa Young Africans umeahidi kufanya usajili utakaowashangaza Mashabiki wengi wa Soka nchini Tanzania wakati wa Dirisga Dogo la Usajili.

Dirisha hilo linatarajiwa kufunguliwa rasmi Desemba 16 mwaka huu kwa timu Shiriki za Ligi Kuu kufanya maboresho ya vikosi vyao.

Young Africans tayari inahusishwa kuiwinda saini ya Kiungo Fundi kutoka nchini Uganda Bobosi Byaruhanga anayemudu kucheza nafasi ya Kiungo Mkabaji na Mshambuliaji sambamba na Kiungo wa zamani wa Azam FC Mudathir Yahya Abbas.

Rais wa Young Africans Hersi Said amesema anaamini wana wachezaji wazuri walio katika ubora, lakini haiwafanyi wasisajili vyuma vingine vyenye viwango vya juu wakati wa Dirisha Dogo.

Hersi amesema kikubwa wanachopanga hivi sasa ni kutaka kuikitisa Afrika kwa kusajili mchezaji Bora wa Afrika msimu uliopita, ili kuhakikisha wanatengeneza kikosi Bora na Imara.

“Lipo wazi Young Africans tuna kikosi bora na imara ambacho kimeweka historia kubwa ambayo haitasahaulika ya kucheza michezo 49 bila kufungwa katika ligi, kitu ambacho sio kidogo.”

Simba SC yafunguka usajili wa Ntibazonkiza

“Licha ya ubora wa kikosi chetu, haituzuii kuendelea kukiboresha kwa kufanya usajili uliokuwa bora na kuongeza ushindani wa namba kikosini.”

“Ninaahidi kuweka historia ya usajili katika Dirisha la Usajili kwa kusajili mmoja wa wachezaji bora Barani Afrika msimu uliopita, tutamtambulisha mara baada ya kukamilisha kila kitu.” amesema Hersi Said

Young Africans imedhamirai kutetea Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2022/23, sambamba na kuvuka hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba SC yaanika wazi hatma ya Enock Inonga
Jumuiya ya Kimataifa yalaumiwa mgogoro wa DRC