Klabu ya Young Africans imepanga kuwarejesha makocha wa timu hiyo Luc Eymael (Kocha Mkuu) na Riedoh Berdien (Kocha wa Viungo) ambao wapo nje ya nchi baada ya selikali kutangaza kuendelea kwa Ligi kuu kuanzia Juni Mosi.

Rais John Magufuli ametangaza uamuzi huo leo jijini Dodoma baada ya kumuapisha Godwin Mollel kuwa naibu waziri wa afya kushika nafasi ya Dk Faustine Ndungulile ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Pia aliapisha mabalozi na katibu tawala mmoja katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans Hassan Bumbuli amesema wamepanga kuwatumia tiketi za ndege makocha hao, baada ya Rais Magufuli kutangaza kuwa ndege kutoka mataifa mengine zitaanza kuruhusiwa kutua nchini.  

“Tumepanga kuwakatia tiketi baada ya Rais kutangaza kuwa ndeg kutoka mataifa mengine zitaanza kuruhusiwa, kwa hiyo tunaangalia ndege gani itamfaa na kocha wetu anaweza kurejea ndani ya siku tatu (3) zijazo ili kuwa tayari kwa maandalizi”-Hassan Bumbuli.

Kuhusu Mlinda Mlango Farouk Shikhalo, Bumbuli amesema klabu ya Young Africans itafanya juhudi zote kuhakikisha anarejea kwa wakati licha ya sintofahamu iliyozuka kwenye mipaka ya Kenya na Tanzania.

Katika hatua nyingine Bumbuli amesema wachezaji wamepokea kwa furaha taarifa za kurejea tena kwa ligi.

“Mwitikio wa wachezaji ni mkubwa kuhusu taarifa za kurejea kwa ligi. Nilizungumza na nahodha Papy Tshishimbi na nahodha msaidizi Juma Abdul, wote wanasema wame-miss kucheza. Bernard Mirrison naye amesema ame-miss kazi.”

Kovu lisilofutika: Miaka 24 kuzama kwa MV Bukoba
Uganda: maambukizi yafikia 274 visa 10 vyaongezeka