Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara amesema bado kikosi chao kina nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, licha ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Young Africans ilipoteza mchezo wa mkondo wa kwanza jana Jumapili (Septemba 12), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kujiweka katika mtihani mgumu wa kusaka ushindi wa zaidi ya mabao mawili kwa sifuri kwenye mchezo wa mkondo wa pili.

Manara ambaye alikua sehemu ya mashuhuda wa mchezo huo Uwanja wa Benjamin Mkapa, amesema bado wana nafasi ya kufanya kwa ajili ya dakika 90 zilizobaki huku akiwaomba mabashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuwa bega kwa bega.

Pia kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram wa Young Africans wameandika ujumbe huu:”Jumapili hii ya 19/9/2021, tunashuka dimbani kwenye mchezo wetu wa marudiano wa kimataifa hatua ya awali dhidi ya Rivers United FC nchini Nigeria.”

“Tutarudi tukiwa imara zaidi,”

Mchezo wa Mkondo wa pili kati ya Rivers United dhidi ya Young Africans utachezwa Jumapili (Septamba 19), Uwanja wa Yakubu Gowon, mjini Port Harcourt katika jimbo la Rivers.

Saba wawania Udiwani CCM Kata ya Ndembezi
Barbara aishauri Young Africans