Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans kinatarajiwa kushuka uwanjani kesho Jumamosi kwa ajili ya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya St Louis kutoka nchini Shelisheli.

Wakati hilo likisubiriwa kwa hamu kubw ana mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe, inafahamika wazi kuwa timu hiyo imezuiwa kuutumia Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kuelekea mtanage huo.

Kupitia ukurasa wa Young Africans wa Instagrama wametoa tamko kwa kuandika hivi:

“Wakati tukijindaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imezuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, na hivyo mazoezi yamefanyika kwenye Uwanja wa Polisi.”

Mbali na hapo taarifa hiyo imemnukuu meneja wa uwanja huo wa Taifa ambapo alisema: “Huu siyo uwanja wa mazoezi ni uwanja kwa ajili ya mechi, lakini kwa kuwa mgeni hajawahi kuutumia kanuni zinasema ni lazima wapate muda wa kufanya mazoezi kabla ya muda wa mechi.”

Kocha wa Yanga, George Lwandamina amelalamikia kitendo hicho kwa kusema siyo cha kiungwana kwa kuwa hata kama Yanga wameuzoea uwanja huo bado wana haki ya kuutumia kwa ajili ya mazoezi.

Naye Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kikanuni wao ambao ni wenyeji, wanaruhusiwa kufanya mazoezi katika uwanja huo ikiwa siku mbili kabla ya mchezo huo.

Saleh alisema walifika uwanjani hapo lakini uongozi wa uwanja ukawazuia kufanya mazoezi wakiwataka kwenda kufanya kwingine kwa hofu ya kuziharibu nyasi.

Watu 7 watiwa mbaroni wizi wa pikipiki
ZESCO wafanya mazoezi kwa siri