Wachezaji na viongozi wa klabu ya Toto Africans wameingia katika vurumai ya wao kwa wao baada ya kikosi chao kukubalia kupoteza mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Young Africans kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Habari ambazo zimezagaa tangu siku ya jumamosi mara baada ya mtanange huoa mbao ulishuhudia Young Africans wakichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja ni kwamba baadhi ya viongozi na wachezaji walituhumiwa kuhujumu timu yao kwa mapenzi waliyonayo dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Kwa nayakati tofauti baadhi ya wachezaji pamoja na viongozi walionekana kulumbana kwa kutupiana lawama kuwa wamepoteza mchezo huo kwa uzembe wao na si kwamba walizidiwa na Young Africans.

Kiungo wa Toto, Abdallah Seseme alisema kuwa ”Inaumiza sana hii ilikuwa ni mechi ya kupatia pesa endapo tungeshinda lakini imekuwa tofauti na unadhani nani atatoa pesa katika mechi zilizobaki hata tukishinda.

”Tungewafunga Yanga tungepata pesa nyingi ndiyo maana wachezaji wamekasirika. Kuhusu hizo tuhuma hakuna mwenye uhakika nazo na malumbano ya viongozi yaliyotokea hayo ni mambo yao wenyewe. Sisi tunasubiri kikao kwani walisema watakuja kujadili na sisi muda wowote tu,” alisema Seseme.

Toto wanajiandaa na mchezo wa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa jijini Mbeya mwishoni mwa juma hili.

Rais wa Korea Kaskazini apiga marufuku Ndoa na Misiba
Wenger Asalimu Amri Kwa Mashabiki Wanaompinga