Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans wamewasilisha barua ya maombi ofisini kwa waziri wa habari, utamaduni, utalii na michezo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, kuomba ridhaa ya kuutumia uwanja wa Aman uliopo mjini Unguja.

Young Africans wamewasilisha barua hiyo, kufuatia marufuku iliyotolewa na waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Nape Nnauye mwishoni mwa juma lililopita kufuatia uharibifu uliofanywa na mashabiki kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mashabiki wanaodhaniwa wa klabu ya Simba waling’oa viti uwnajani hapo kwa madai ya kuchukizwa na maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya timu yao wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Young Africans.

Katika barua ya Young Africans ambayo imesainiwa na kaimu katibu mkuu Baraka Deusdedit, wamemuhakikishia waziri wa habari, utamaduni, utalii na michezo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwa, michezo yao yote itachezwa katika uwanja wa amani endapo ombi lao litakubaliwa.

Kwa mantiki hiyo sasa inadhihirisha kuwa, Young Africans watacheza michezo yao ya ligi kuu ya soka Tanzania bara katika ardhi ya visiwani Zanzibar.

yanga

Waziri Mkuu akutana na Mwenyekiti baraza la UDOM
Mario Balotelli: Simfahamu Jurgen Klopp