Mabingwa wa soka Tanzania bara, Young Africans  wameondoka Saa 10:00 alfajiri ya leo kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Township Rollers utakaopigwa Jumamosi mjini Gaborone.

Jumla ya wachezaji 20 na viongozi 11 wakiwemo wanane (8) wa benchi la ufundi ndiyo waliounda msafara wa timu hiyo, huku tiketi 150 zikitolewa kwa ajili ya mashabiki watakaoingia kwenye Uwanja wa Taifa wa Botswana kuiunga mkono.

Katika mchezo huo Young Africans wanahitaji ushindi wa ugenini wa 2-0 ili kwenda hatua ya makundi baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kimeondoka ikiwa ni saa chache baada ya kuendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia kuichapa Stand United mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Yanga chini ya kocha George Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali kufikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.

Rais Kiir amtimua waziri wa fedha na ofisa wa jeshi
Video: Abdul Nondo alijiteka mwenyewe- Kamanda Mambosasa